KUNA redio moja ya kidini inayotangaza kutoka Morogoro ambayo isipojiangalia itakuta inajiabisha siku hadi siku.
Jumamosi tarehe 7, Januari 2011 Redio hiyo ilikuwa na mahojiano na mwanasheria ambaye pamoja na kuwa hajui uandishi na uhariri wa habari unavyofanywa anakosowa waandishi wa habari.
Kubwa zaidi, hata hivyo, mwanasheria huyo tofauti na vigogo wa sheria nchini eti yeye kamuelewe rais kutaka kufanya marekebisho ya katiba na sio kuundwa kwa katiba mpya. Mmh.....kuna lao jambo.
Ni redio hiyo hiyo iliyomripoti Ndugu Issa Shivji kinyume kwa kusema eti amekataa kutungwa kwa katiba mpya. Jamani, endapo hamlitaki jambo kwa sababu zenu wenyewe msiwawekee watu maneno mdomoni. Sidhani kama Uislamu unakubali hilo. Unafiki na hasa redioni hauchelewi kuumbulika.
Tafuteni wahariri wa kiislamu (ambao wapo) wawanoeni ili mjenge Credibity kwanza kabla ya mambo mengine la sivyo watawasikiliza wengi leo, lakini kesho mtajikuta mnatangazia upepo nchi nzima!