Hivi unaweza kuwa na gazeti ambalo halibadili maudhui wala sura yake kwa miaka 2-3 na bado ukaamini unaweza ukashindana kwenye soko kwa kuuza jina la zamani tu?
Jiulize, tuwasiliane, tuongee na tufanye kazi! Bado kuna soko zuri tu mtu ukijiweka sawa kuanzia sasa maana msisimko wa demokrasia na katiba utazidi kuongezeka siku hadi siku!
USHAURI kwa vyombo vya habari tanzania. Ikiwemo magazeti, redio, televisheni, tovuti na midia mpya kwa nia ya kuboresha kile wakipatacho wasomaji, wasikilizaji au watazamaji. Wasiliana nami kupitia SMS: +255714265218.
Tuesday, April 19, 2011
Taarifa za Habari za dakika 10 zimepitwa na wakati
Mtanisahihisha kama ninakosea. Lakini ninaamini taarifa za habari za dakika 10 katika redio ni jambo lililopitwa na wakati.
Yapo maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi yenye masuala mbalimbali yanayoweza kuwa chachu ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiteknolojia na kiutamaduni endapo yanazungumziwa kwa kina na kwa upana wake na Watanzania wakajifunza kitu hapo na hivyo taarifa ya habari yenye uchambuzi wa dakika 20 au zaidi nadhani ndiyo iwe staili ya taarifa zetu za habari kuanzia sasa.
Ni bora uwe na taarifa mbili au tatu tu za habari kwa siku kuliko kuwa na taarifa 6 au zaidi ambazo hazina lolote jipya na ni za dakika chini ya 10 kila moja!

Redio za dini na siasa
HAKUNA hatari kubwa kama ile ya chombo cha habari cha kidini kuchanganya siasa na dini. Kumbukeni kina Radio Quran, Radio Kheri na Radio Imani yale ya Redio za kule Rwanda jamani!
Kama mpenzi wa redio hizo za dini hapo awali nilicacha kuzisikiliza kabisa zilipoanza kuhubiri siasa na tena zikionesha kuegemea waziwazi upande mmoja. Sikuhizi ninazisikiliza tu pale ninaposikia Kurani Tukufu inasomwa. Basi!
Wale wanaohusika na usimamizi wa vyombo vya habari watupie macho vyombo hivi kwa sababu kwa kweli kitaalamu na kimaadili vinahitaji msaada mkubwa tena wa haraka!

Mmm, Watangazaji kama hawa !
Unapomsikia mtangazaji wa redio au televisheni anayeshindwa kutofautisha kati ya 'ri' na 'li' katika kiswahili na wala sio Kiingereza, je, unakichukulia vipi chombo cha habari husika?
Subscribe to:
Posts (Atom)