Wednesday, September 8, 2010

TBC na Osibisa.

Kufuatia msiba wa mmoja wa waanzilishi wa bendi ya Osibisam Mac Tontoh [69], wenzetu
wa TBC walifanya kazi nzuri ya kuichambua historia ya kundi hilo lililoitambulisha
Afrika kwa dunia kunamo miaka ya 70 hadi kunyauka kwake mwanzoni mwa 90.

Katika maombelezo hayo TBC pamoja na mengine ilitoa changamoto la muziki unaotumia
ala halisi za muziki na umuhimu wa kuwa na chuo cha kufundisha vijana wetu upigaji
ala za muziki asilia na zile za Kizungu na nyinginezo tokea nchi mbalimbali duniani
ili kuwa na muziki tajiri badala ya muziki wenye mahadhi na mdundo wa kurekodiwa
unaofanya muziki wa Afrika kuwa kichekesho duniani tofauti na muziki wa Osibisa
uliokuwa tishio kwa miziki mingine duniani.

Ninaamini TBC na wadau wengine sasa watakwenda hatua moja na kuanzisha chuo cha ala
za muziki ili kunusuru kizazi hiki na muziki wa elektroniki usiyo na asili wala

Redio zote za FM

Karibia redio zote za FM Tanzania zina matatizo wakati wa kuwasiliana na watu nje ya
studio kwa simu. Makelele mengi husikika na ni kawaida ya watangazaji kuwashurutisha
wasikilizaji kupunguza sauti ya redio zao. Je, hii ni sahihi ?Au na redio kama sekta
nyingine tunakuwa ni wale wale waswahili wa kuachia matatizo kuwa matatizo mwaka
nenda, mwaka rudi. Hangaikeni kutafuta teknolojia maridhawa na isiyoingilia uhuru wa
wasikilizaji nadhani na ninaamini ipo....hatujajishughulisha vya kutosha tu !!!

FM 100.5

Ninaomba kazi toka kituo hiki ambacho kuamkia usiku wa leo kuanzia saa tisa usiku
hadi ninapoandika hili karibu saa 11 asubuhi kompyuta ilikuwa imejamu na sauti
iliyokuwa ikitoka ni nkidu nkidu nkidu nkidu nkidu....

La, sivyo wawafundishe hata walinzi kuishtua basi kompyuta inapojamu. Ni redio yenye
jina kubwa na kosa la namna hii halistahili kuwepo kamwe. Je, hakuna radio monitors
ndani na nje ya studio? Je, hakuna mtangazaji wa zamu usiku (mtu ambaye kukaa macho
usiku kwake si taabu au starehe).