Mtanisahihisha kama ninakosea. Lakini ninaamini taarifa za habari za dakika 10 katika redio ni jambo lililopitwa na wakati.
Yapo maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi yenye masuala mbalimbali yanayoweza kuwa chachu ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiteknolojia na kiutamaduni endapo yanazungumziwa kwa kina na kwa upana wake na Watanzania wakajifunza kitu hapo na hivyo taarifa ya habari yenye uchambuzi wa dakika 20 au zaidi nadhani ndiyo iwe staili ya taarifa zetu za habari kuanzia sasa.
Ni bora uwe na taarifa mbili au tatu tu za habari kwa siku kuliko kuwa na taarifa 6 au zaidi ambazo hazina lolote jipya na ni za dakika chini ya 10 kila moja!
No comments:
Post a Comment