HAKUNA hatari kubwa kama ile ya chombo cha habari cha kidini kuchanganya siasa na dini. Kumbukeni kina Radio Quran, Radio Kheri na Radio Imani yale ya Redio za kule Rwanda jamani!
Kama mpenzi wa redio hizo za dini hapo awali nilicacha kuzisikiliza kabisa zilipoanza kuhubiri siasa na tena zikionesha kuegemea waziwazi upande mmoja. Sikuhizi ninazisikiliza tu pale ninaposikia Kurani Tukufu inasomwa. Basi!
Wale wanaohusika na usimamizi wa vyombo vya habari watupie macho vyombo hivi kwa sababu kwa kweli kitaalamu na kimaadili vinahitaji msaada mkubwa tena wa haraka!
No comments:
Post a Comment